Maisha yetu huingiliana kupitia chakula – kupanda, kukusanya, kuuza, kununua na kwa mlo. Wengi wetu huwa na kumbukumbu kuu zinazohusiana na chakula – mlo wa sikukuu pamoja na familia na marafiki, harufu za vyakula vipendwavyo au mafunzo ya upishi wa resipe ya familia. Soko huwapa wahamiaji vyakula vinavyowaunganisha na kumbukumbu za nyumbani kwao, mila zao na utamaduni wao katika nchi mpya.
Nataka kufanya kile ambacho watu wanahitaji. Hawa watu ni kama wale walio njaa. Unajua hata mimi nikikipenda chakula cha nchi yangu na nikikose, nitahisi kama yule ambaye hana chakula. Mimi hujaribu vyakula vya aina mbali mbali lakini huwa sishibi. Hawapati chakula cha kwao lakini kwa vile niko hapa, nawasaidia. — Goma Khadka, mmiliki mwenza, Soko la RGS Nepali, Burlington
Ndugu yangu alikuwa anaongea kuhusu kuingia ndani ya duka la Merola mtaani kwake, au duka la Izzo. Aliongea pia kuhusu aina mbali mbali za jibini kutoka Italia. Bidhaa zote zilioka Italia na wangeleta bakuli kuu za pweza wakati wa Krismasi. Na angesema hata umfunge macho na umpeleke kwenye duka lolote, angeweza kukuambia yuko wapi kutokana na harufu za jibini na nyama zilizokatwa. — Michel Allen, mkaazi wa Burlington kutoka Lebanon.
Soko za awali zilikuwa zinauza vyakula vya kawaida vya Marekani, ambavyo vingetumiwa kupika vyakula vya tamaduni kadhaa – vyakula vilivyohifadhiwa kwenye makopo au kukaushwa, nyama, bidhaa za maziwa, na mboga. Soko zilizowauzia Wayahudi zilikuwa jambo la kipekee. Siku hizi, soko huuza bidhaa zinazotumiwa katika vyakula vya bara la Asia, Afrika, na Ulaya ya Mashariki – matunda na mboga, viungo, vitoweo, samaki, na nyama.
Wanunuzi hujali kuhusu asili ya vyakula vyao. Wateja Waafrika wa soko la RGS Nepali hupendelea samaki iliyokaushwa inayopatikana kutoka kwa sehemu maalum ambazo wanazitambua. Wanunuzi kutoka Poland katika soko la Euro wanataka soseji ya kielbasa inayotoka Poland. Wateja wa Community Halal wanapendelea ladha ya nyama halal iliyotoka Australia. Wenye soko wanaelewa umuhimu wa matakwa ya wateja wao na wanatumia masaa mengi kutafuta
bidhaa hizi.
Katika majira ya baridi, kila mtu alitengeneza mikate ya nyama. Baba yangu alikuwa anasiaga nyama. Mikate hii ilikuwa ya Kikanada na iliundwa na nyama ya ng’ombe na nguruwe. Mama yangu alishughulika na jibini ya kichwa. Katika muda huo, ilitengenezwa kutoka kwa kichwa cha nguruwe. Hiyo ilikuwa mila, pamoja na ile boudin, ambayo ni soseji ya damu. Baba yangu alikuwa anaitengeneza mwenyewe kwenye dukan a kuiuza. — Val Sicard, bintiye Donat Danis, wa Danis’s Market, Burlington.
Ingawa haitoshani ukubwa na haileti pesa kama ile ya Iraq, inawakumbusha wateja wangu kuhusu nyumbani kila wanapoingia na kuona bidhaa za Kiarabu. Inawasaidia kupata utamaduni wao na wanajua ya kwamba wanatoka mahali, hata kama ni duka ndogo tu. — Bintiye Ahmed Aref, meneja wa soko ya Nada International, Winooski.
Ninapoenda kwenye soko kuu la kawaida, huwa sipati vyakula vya Kiafrika ambavyo navihitaji. Inabidi niende kwa duka la Nepali, Afrika au la Kisomali ili nipate vyakula ninavyohitaji. Kwa mfano, hapa wana nyama halal, mimi ni Muislamu na siwezi kuila nyama yoyote ingine. – Zeynab Kouate, mnunuzi, duka la Community Halal, Burlington
Wamiliki wa soko hufanya kazi kwa wingi ili kupata vyakula vinavyoitishwa na wateja wao. Lugha ikiwa kikwazo, wamiliki hutumia picha wanavyopewa na wateja wao kutafuta kwenye mtandao na kuonyesha wauzaji wa jumla na soko katika miji kubwa. Wamiliki wengi husafiri kwa muda mrefu kuchukua bidhaa mara kadhaa kila mwezi kwa sababu ya bei na vikwazo kwa utoaji hadi Vermont.
Wamiliki wa kitambo waliagiza bidhaa maalum kutoka kwa majiji makuu lakini walinunua bidhaa Zaidi kutoka kwa shamba, duka za mikate, duka za nyam ana wasambazaji wa vinywaji vya karibu. Wanajamii pia walirudi na vyakula kila walipotembelea jamaa zao kwenye miji kuu kama New York, Boston na Montreal.
Tulifanya utafiti, kama kuuliza mteja, “Umetoka eneo gani Afrika? Kongo? Umetoka Burundi? Umetoka Togo?” Sisi hujaribu kukusanya taarifa nyingi iwezekanavyo kutoka kwa watu wengi kuhusu vyakula ambavyo wanavila na tunajaribu kuvipata. — Ratna Khadka, mmiliki mwenza, Soko la RGS Nepali, Burlington
Ni mkate yetu ya kitamaduni tu, mkate tuliyoila tukitembea kwenda shule. Kwenye jiji, tulikuwa na duka za mikate ambapo tulienda kununua. Duka hii ina kumbu kumbu mengi. — Dado Vujanovic, mmiliki, Euro Market, South Burlington
Katika nusu ya kwanza ya karne hii, soko zilikuwa zimejaa Winooski na Burlington. Wakaaji walitembea maeneo ya karibu ili kufika sokoni. Kwa sasa, soko zimeenea zaidi na watu wengi wanahitaji usafiri wa umma au gari kuzifikia – kikwazo kwa Wamarekani wapya wengi.
Kama Wanavermont wengi, wahamiaji hupanda mboga na matunda katika shamba za nyumbani kuongezea wanachonunua dukani. Wengine wao hupanda vyakula wanavyotambia katika mashamba zinazosimamiwa na New Farms for New Americans. Tabia hii ya kueneza mavuno ya ziada kwa wanajamii inaendelea hapa.
Wengine wameanzisha shamba ndogo na biashara za kuagiza ili kuletea jamii zao vyakula muhimu kama biriganya na bidhaa za mihogo.
Mojawapo ya sababu nilichagua kubaki Vermont ilikuwa kuwepo kwa soko la Nada International vile vile soko la Kiafrika ambapo ninaweza kununua vyakula vya nyumbani. Niliishi Pennsylvania kwa miaka miwili lakini nilitoka kwa sababu sikuweza kupata mahali ningeweza kununua vitu kama hivyo. —Goma Mabika, mteja, Winooski
Nilichagua jordgubbar, maharagwe na mbaazi kwa wingi. Nakumbuka nikijaza kikapu kubwa na kuileta dukani. Baba yangu aliyekuwa na maandishi mazuri angeandika vibaoni, “maharagweyaliyopandwa nyumbani.” —Louis Mario Izzo, kuhusu shamba la nyanyake Concetta, Burlington
Kwa kweli ni mmea wa ajabu. — Musiya Mutume, mmiliki, M. Square Vermont, Winooski
Tamaduni za upishi husafiri na wat una kuingia nchi mpya. Mihogo, iliyoasilia Marekani Kusini, huliwa kwa wingi Afrika na Asia. Majani yake hutumiwa kwenye vitoweo, mizizi yake kutengeneza unga au kuchemshwa au kuchomwa kutengeneza chakula kilichojaa kabohaidreti.
Green Mountain Cassava kutoka Vermont husambaza mihogo kwa soko kadhaa.
Huko Afrika, unaponda majani ya mihogo hadi yawe laini. Wamejifunza kuyafunga kwenye friji na kuyauza hapa. Yanaonja kama ya nyumbani. — Faraja Achinda, mteja, M. Square Vermont, Winooski
Nyama ya kondoo na kwanga, mkate ya mhogo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika M. Square Vermont
Jamii ya Kilebanon waliagiza bidhaa kutoka Brooklyn, New York, kupitia mfumo wa barua. Ilikuwa inaitwa Sahadi Company. Nakumbuka mfumo huu ikiwa na bidhaa za kipekee. Familia waliagiza walichohitaji na kikasha kikubwa kingefika. — Monica Simon Farrington, mkaazi wa Burlington kutoka Lebanon
Napenda kununua hapa. Familia ni nzuri ajabu – nawajua kibinafsi – usafi wa bidhaa anazoleta kutoka kwa miji kuu ambapo panapatikana viungo vya Kiasia na kwa wingi. Si Kivietnamu pekee, ni vya Kijapani na Kikorea Kusini. —Peter Maisel, mwenye mkahawa na mnunuzi, Thai Phat, Burlington
Kibbeh ya Kilebanon hutengenezwa kutoka kwa nyama ya ng’ombe au kondoo iliyosiagwa, nafaka ya bulgur, vitunguu, na viungo. Huwa inakulwa mbichi, so ni muhimu kutumia nyama safi isiyo na mafuta.
Alikuwa anaenda nyuma ya kaunta na kwenye friji na kuja na nyama ya ng’ombe cha kiasi kubwa. Angeiweka kwa meza ya mbao na kuvinoa visu vyake. Siri yake ilikuwa kusiaga nyama mara mbili, iwe laini vilivyo
—Monica Simon Farrington, mnunuzi wa asili ya Lebanon, soko la George, Burlington
Baba yangu alikuwa ananunua bidhaa huko North Street. Kulikuwa na duka nyingi za Kiyahudi. Nadhani baba alipendelea kufanya biashara na Wayahudi kwa sababu walikuwa wamekaribiana kiutamaduni, walielewana na waliweza kuongea kwa urahisi. Alikuwa rafiki kwao. —Michel Allen, mkaazi wa Burlington kutoka Lebanon
Unaweza kutembelea wakati wowote, sio lazima hata ununue chochote, unaweza kupumzika tu kwenye duka, chochote, ni kama nyumba nyingine, kuwa waaminifu. Inahisi kama ninaingia tu nyumbani kwangu, unajua ninachosema? —Emmanuel Braxton, mteja, Soko la RGS Nepali, Burlington