Ukija dukani ambapo hupati shida ya mawasiliano na unaweza kuitisha unachokitaka na mmiliki ataelewa, vitu vinakuwa sawa. — Mahadi Hassan Moussa kuhusu Community Halal Store

 

Yeyote ambaye amefungua biashara amefungua kwa familia yake au kupata pesa zake. Lakini familia hiyo husaidia kila mtu. Kwa hivyo, si duka tu. Ni duka la jamii. —Ahmed Omar on Community Halal Store

 

Ndoto yangu, tangu niwe mchanga, imekuwa kujifanyia kazi. Nilitaka kufanya hivyo ili niwe huru na niweze kujikimu pamoja na jamii yangu. Nimepitia ugumu kwani imenibidi kutia bidii ilhali nimeajiriwa katika kazi mbili tofauti mfululizo
— Muyisa Mutume, mmiliki, M. Square Vermont

 

Vermont ni kuzuri mno na ni vyema kuja na kutangamana na utamaduni mwingine. Hata hivyo, kuwa na mahali ambapo panaweza kukumbusha kuhusu nyumbani pana umuhimu, na kukosa hicho eneo hili kunatisha. —Faraja Achinda kuhusu M. Square Vermont

 

Nashukuru jamii yetu kwa kutusaidia katika hii safari. Pande zote mbili zimefaidika, na niko hapa kwao, lakini hakuna kitu ambacho kingewezekana bila wateja wangu. Nashukuru tu, nchi ambayo nimetoka na sasa ndoto yangu imetimia.
—Dado Vujanovic, mmiliki, Euro Market

 

Kikawaida, ilibidi twende hadi Kanada kununua bidhaa, lakini tangu wafungue soko hii katika msimu wa Covid, mambo yameboreka kwetu. Wanatuuzia bidhaa bora kama nyumbani. —Francis Mabawidi kuhusu M. Square Vermont

 

Wakati wowote mteja anapoingia dukani, namuuliza, “Unapenda nini?” Ananiambia, “Napenda hiki ama kile,” nami naleta kitu hicho. Hata kama kinatoka kwa jimbo lingine, nakiagiza, nakitafuta kwenye Google, mahali popote kilipo, ninakipata na ninakileta. Naleta hadi mafuta ya mhogo. Kila kitu. —Ahmed Aref, meneja, Nada International Market

 

Sote tuko hapa kutafuta maisha bora, ndoto, na tunahitaji kusaidiana vilivyo. Nilikuja hapa nikiwa umri wa 18 kama mhamiaji na nikawa mwananchi. Nahisi uhusiano kwa sababu najua walipopitia walipokuja hapa. —Isela Marin O’Brien kuhusu RGS Nepali Market

 

Huu ndio utofauti ambamo nchi hii umejengwa, na hawa wageni wanaleta utamaduni mkuu. Kile ambacho wanakileta inatajirisha Marekani. Watu hawa ni Wairaki lakini wanaleta vyakula kutoka kwa maeneo yote ya dunia, kutoka kwa dunia yao. Soko hizi ni kuu, ni rembo, nazipenda mno. —Asiyetambulika kuhusu Nada International Market

 

Mradi wa Zaidi ya Soko ulitokana na mbinu ya uchunguzi inayoitwa ethnografia shirikishi. Kuanzia usanifu wa mradi hadi kazi ya shambani ili kuonyesha maendeleo, tumejaribu kuelewa uzoefu kutoka kwa mtazamo wa wale ambao uzoefu huo ni wao. Maamuzi yalifanywa kwa ushirikiano na wamiliki wa soko na wateja. Katika hali zote, tumefuata mwongozo wao na matakwa yao, ili kuchangiza maneno yao na kuonyesha picha zao, au majina-au sivyo-walivyochagua. Waandishi wa mradi huu ni watu ambao maneno yao na nyuso zao unaziona hapa.

Tunatumia neno “mhamiaji” na “mkimbizi” kwa sababu ni ya kweli, yanayoelezea jambo la zamani-kuhama kwa hiari au kulazimishwa kwa watu, kote ulimwenguni. Neno “Mmarekani mpya” ni sawa kwa wamoja, lakini halifurahishi kwa wengine. Kwa maneno ya mmoja wa washirika wetu na wamiliki wa soko. Kuitwa Mmarekani “mpya” kunasikika kama kushushwa kwenye kategoria tofauti ya Mmarekan